KUTOKANA NA MASWALI KUWA MENGI JUU YA HII SHUGHULI YA SINGO NAOMBA NITOE UFAFANUZI KUTOKANA NA UELEWA WANGU MIMI, THEN YEYOTE ATAWEZA ONGEZEA YEYE ANAVYOIELEWA ILI SOOTE TUELEWE HII NI SHUGHULI YA AINA GANI MAANA WATU IMEWAMIX MAANA WANAMSAKA BI HARUSI HAWAMUONI WANAISHI DHANI NI NDOA ZA AINA NYENGINEZO
SINGO INATOKANA NA NENO KUSINGWA.... NI SHEREHE AMBAZO BI HARUSI AU BWANA HARUSI ANASINGWA....KUSINGWA ANASUGULIWA NA AINA YA MAJANI YANUKIAYO MWILINI(WAZANZIBAR WATAKUWA WANAJUA HATA AINA GANI YA MAJANI ILA ME NAJUA NI MAJANI MAKAVU YAKIWEPO YA MLANGILANGI,ASUMIN NA LIWA NK) ....HII SI KWA MAHARUSI TU BALI HATA WEWE MDAU WAWEZA SINGWA AU UKAMSINGWA MUMEO...ILA KUTOKANA NA WATU KUTOKUWA NA UTAMADUNI WA HAYA MAMBO NDO INAANDALIWA SIKU SPECIAL KWA MTARAJIWA KUSINGWAA...
.KWA WATU WA PWANI WENGI WANASINGWA MFANO MUMEO HAYUKO ANAREJEA SO WAENDA SINGWA WENGINE WANASINGWA SIKU ZA SHEREHE MAALUM KAMA EID AU SIKU ZAO ZA KUZALIWA ....kwa kizungu nadhani ni vile mnafanyiwa spa, body srub na massage....kuSafishwa ngozi ambako ni zaidi ya kuoga maji .....ILA HII SABABU INAKUWA KWA SIKU MAALUM BASI NDO TUNAIFANYIA SHEREHEE... MFANO HII SINGO YA
BWANA MOHAMED....
.ILIFANYIKA NYUMBANI KWAO AMBAKO BWANA HARUSI NA WAPAMBE WALISINGWA .....KISHA WAKAJA UKUMBINI AMBAKO YALIENDELEA HAYO YA PICHANI
NOTE:: WENYEWE WATU WA PWANI HILI SINGO LINAANDALIWA NA BIBI (wale wanaowaita waoaji mume mume hivyo humfanyia iyo kama kumkosha akapate jiko) HATA SHANGAZI ANAWEZA MFANYIA MHUSIKA sema siku hz kimjini mjini ndo INACHAKACHULIWA KISTYLE
NI HAYO...NAWE MDAU UNAEJUA SINGO NI NINI TUELEZEE 2FAHAMISHANE
No comments:
Post a Comment