Wednesday, January 20, 2010

MJADALA::KUBADILISHA MATRON


MASHOST LEO HEBU TULIJADILI HILI

Siku za karibuni nimeona Baadhi ya sherehe maharusi wakiwa wamebadili matroni yaani mtu anakuwa na matron wa kitchen Party, Sendoff na wa Ndoa

Hebu mnijuze ni fashion au kuna kitu gani kinatokea hadi kupelekea Bi harusi mmoja kubadili matron kwa kila sherehe na ashindwe chagua mmoja ambaye atamsimamia katika sherehe zote...kama enzi zetu sisi

Na mkumbuke kuna wengine hawana matron katika baadhi ya sherehe kama Send off na Kitchen party... lakini hili TUPA KULE...TULISHALIJADILI


15 comments:

Anonymous said...

Hili ni kweli. Ila mie sababu yangu ilikuwa ni kwamba nina mashoga watatu. Na kila mmoja nilitaka aone kuwa ana umuhimu kwangu. Therefore nikawapa wote chance ya kuwa made of honors.MMoja k/party, wa pili sendoff, na mwingine kwenye harusi.

Anonymous said...

Ili kupunguza gharama na mzigo kwa matroni kununua nguo na viatu mara tatu, kwa maisha ya bongo sio rahisi mtu akaweza kununua vitu vya sherehe tatu kwa mara moja.

Anonymous said...

ni kweli gharama ni kubwa kuwa na matron mmoja tu inategemea na uwezo wake kifedha.

Anonymous said...

availability of the person also matters.

Anonymous said...

na sisitiza hapa kwa matron ni afadhali wangekua wanachukua rangi kidogo inayo ingiliana na mtarajiwa ili isi fanane kila kitu mimi naona kama hapa matroni kapendeza kuzidi biharusi sasa hii sio nzuri angechanganya rangi nyingine kidogo ili kutofautisha sana na mtarajiwa ili iwe siku yake tu sio mtu unatamani sijui umchague nani.na mimi nafikiri kitchen party mtu unakua peke yako send off unachagua eidha uwe na mtu au usiwe nae yote ni ubunifu unatakiwa.mitindo ipo kwa mustafa,naledi,na wengine ukicheki utapata nguo nyingi za kitchen party kila siku nguo kama za send off zina chosha.

Anonymous said...

mamboz wanablog!! mimi napenda kazungumzia kwa upande wa wakristu, utakuta mtu anapenda shoga yake amsimamie kwenye sherehe zake labda zote tatu lakini kwa ndoa inakuwa inashindika labda kama huyo shoga yake hajaolewa so inakuwa ngumu, kwa sababu msimamizi wa harusi kwa baadhi ya makanisa anatakiwa nae awe na ndoa!! so mtu anakuwa ana matron wa send off na k. party na wa harusi mwingine.

Anonymous said...

sometimes matron uliyemchagua kwa kpat hana nafasi ya kuwepo kwenye harusi au Soff kwa either safari za kikazi au kama harusi inafanyika mkoa tofauti na ilipofanyika kpat au Soff. Lingine matron unayemtaka anaweza kuwa hajaolewa hivyo akashindwa kukusimia harusi especially kwa makanisa ambayo hayakubali So unakuta mtu ana matron tofauti.

Anonymous said...

kwa upande wa matron siku harusi ni lazima awe na ndoa, sasa unakuta labda alo tayari kukusimamia siku ya harusi yupo tight si mnajua mambo ya bongo tena, mishe mishe kibao, hawezi kukusimamia siku zote tatu, ndo mana utakuta wengi wanabadilisha ma-matron mana kwenye k/pati na sendoff ndoa si lazima sana, ni kwamba tu upate mtu wa kukupa tafu pale mbele, nadhani kwa kukwepa gharama ndo mana wengine wanaamua kusimama peke yao kwenye k/pati na sendoff, kwenye harusi ndo utakuta yuko na msimamizi, ila inataka moyo...
kuwa peke yako pale mbele

Namkunda said...

Mi naona ni vizuri kubadilisha inakuwa na sura tofauti na zamani tunaenda na wakati na pia inapunguza gharama za nguo na viatu mana kitchen part lazima uonekane tofauti na sendoff hivyo hivyo kwa hiyo wakiwa tofauti inakuwa nafuu zaidi

Anonymous said...

kwa upande wangu sioni umuhimu wa matron kuvaa almost sare na mwenye harusi.

kwa kweli naona haimpi nafasi ya ku-shine biharusi peke yake.

its her day and she should be the center of attention, y think of looking like cinderella when there will be two cinderellas around?

Anonymous said...

bongo si mnasemaga mna hela za kumwaga, sasa kwa nini mnapunguza tena gharama. i am assuming the lady is in bongo, maana maulaya kwenu huko hakunaga shughuli nyingi ivo. ni bridal shower na arusi thats it

Anonymous said...

Ya. Hilo la garama nakubaliana nalo, na hata hilo la kuonyesha umuhimu wa watu pia nakubaliana nalo.

Anonymous said...

mi nadhan kikubwa ni gharama,maisha yanazid kuwa magumu mambo mengi sn siku hzi na hizi shughuli ndo usisemekila mtu anataka mchango

Sidhani kama mtu anapenda kuchukua matrons wtofauti kiasi hicho manake kuna wale unakuta hawajaolewa basi wanasimamia send off na kitchen party, harus inabd kubadilsha lakin ingekuwa inawezekana unaweka huyo huyo

All n all mi nadhani ni kupunguza gharama

Anonymous said...

mh kazi sana, harusi za siku hizi?

Anonymous said...

nafikiri watu wanapoteza maana halizi ya sherehe hizi,
Mimi nasema ukweli mtupu, atakaechukia na achukie tu wala sitajali mradi nimesema.
wote wanaobadilisha wasimamizi, wanachemsha
hakuna cha gharama wala nini, tusipotoshane hapa, matroni anatatakiwa kuwa mmoja tu!, kitcheparty, sendof na hata harusi, sio siku hizi watu wanajibunia tu! utakuta kitchepart mtu anasimamiwa na mtu ambae hata hajaolewa, au unakuta harusi mtu anasimamiwa na wanandoa tofauti, ili iweje sasa?? mh hizi fasion siku hizi ni too much.
INAPENDEZA UKIWA NA MSIMAMIZI MMOJA TU!

MJADALA::-ETI MATRON AWE MBAYA ILI ASIKUFUNIKE!!

MJADALA::-ETI MATRON AWE MBAYA ILI ASIKUFUNIKE!!

ETI BI HARUSI UNAAMBIWA UCHAGUE MATRON MBAYA INAHUSU? KISA ETI ILI ASIKUFUNIKE KWENYE HARUSI, KWANZA UNAANZAJE? UNA KIPIMO KIPI CHA KUONA WE MZURI ILI YE WE MBAYA?(mbaya afananaje???)

JAMANI MIE NAONA TUACHE UOGA NA TUJIAMINI HADI UMEVISHWA PETE..UMETOLEWA POSA, VIKAO VIMEKAAA HADI SIKU YA SHEREHE BADO MTU HUJAJIAMINI KUWA WE NI BI HARUSI TU ...KIASI KWAMBA MNAFIKIRIA ETI NITAFUTE MATRON MBAYA ANISISAMIE...AAAAA MASHOST HAILETI TAMUUU HEBU TUJIAMINI KUWA SISI NI MABIHARUSI NA HAKUNA KITAKACHOBADILISHA HILO...SI MAKE-UP WALA NGUO

SIKU YANGU HARUSI ..NILIMFIKIRIA MATRON AMBAYE TUKIKAA PALE MBELE TUTAPENDEZA WOOTE, TUTAKUWA HATUBOREKI AT LIST TUWE TUNABADILISHANA MAWAZO NA KUCHEKA INAPOBIDI....HAYA KISA CHA KUMKURUPUA MBIBI UKAMUITE MATRON UNAFIKA PALE MBELE WOTE MMENUNA ...INAHUSUUUUU?!!!

mie yangu hayo SIJUI nyie wadau mwaonaje?!!

NA HUYO NDO ALIKUWA MATRON WANGU NA MAIDS...HAKUNA MBAYA HAPO NA SIKU YANGU ILIENDA VYEMA NA HADI LEO NIPO NDOANI

24 comments:

Anonymous said...

Sio kwamba ni kutokujiamini bali pia ni mtazamo wa watu, harusi ni watu mie sawa bi harusi natakiwa nipendeze zaidi yake sio yeye watu wote ndo wamuangalie ndo maana hata salon huwa wanauliza bi harusi ni nani kati yenu ili wakushughulikie wewe zaidi. Kwangu matron mzuri kunishinda ni big NO hata house girl home pia anatakiwa awe wa level fulani hivi sio watu kutuchanganya

husnaty said...

my dia,matron wako ni mzuri kwa kweli ila hakupendeza kivile,tunaposema kuchagua mzuri ni mambo kama hayo yeye ni mzuri lakini hakuvaa vizuri so tofauti yabaki palepale hajakufunika.....ni maoni tu

Anonymous said...

yeah ni kweli kabis awatu huwa wan fikra mbovu sana si unaona dada yetu alivyopendeza na wapambe wake wote wako bomba,tatizo sisi wanawake wa kibongo wengi wetu hatujiamini mtu pete umeshavishwa na bado hujiamini jamani mpaka unataka uchague matron unaezani si mzuri.tubadilike,lingine dada shamimu mimi binafsi hapa bongo sijawahi ona matron kavaa nguo fupi hivi haiwezekani ama ndio tamaduni zetu?

Anonymous said...

siombaya ilipendeza kunawatu wanatamani hata kama hiyo hawipati mtu inabidi uridhike na ulicho nacho ukitamani basi hata huyo uliye nae unaweza kumuona mbaya uvumili nakujipa moyo kuwa hata wako ni mzuri zaidi ndio utafanikiwa kupitwa na mjaribu tena utviona vya kawida mimi ndio naishi kwa staili hiyo nanina mafanikio.ipendeze isipendeze lakini siku imepita huezi rudia naukirudia haifanani.mdau fingland

pam said...

aaaaah Shamimu inamana wee hujui kuangalia nani ni mrembo nani wa kawaida nani hana mvuto hiyo ipo tu na kila mtu analielewa hilo tho kila mtu ana uzuri wake but kuna general urembo...
Ok abt mada ya kutozidiwa na urembo wa Matron haimaanishi kwamba awe mbaya kwani ni kweli utaharibu muonekano wenu but cha kwanza angalau muwe mnaendana yaani kama ni marafiki basi muwe mmeshawahi kuambiwa kama mwafanana inakuwa bomba zaidi na asiwe anawakaaaaaaaaaa kukuzidi itafanya 1 st sight ya mtazamaji iende kwake na kuishia kukoment mmh mbona kama huyu ndo alipendeza akawa bi harusi sasa kwa kuwa ile ni siku yako you have to be the quenn

Mama naseer said...

shamimu inaonekana harusi yako ilipendeza yaan hapo umependeza shela imetulia kwenye figure i would like to see more picture of ur wedding,u guys looking good

Anonymous said...

you look great zeze, nguo yako nzuri na ulipendeza sana, kama hutojali naomba kufahamu uliolewa lini. Pia post picha nyingine za harusi yako jamani unajua ina raha kwa sisi ambao tnapenda blog yako kukufahamu kiasi na ntashukuru kama utakuwa unatu update kuhusu mtoto wako hasa kwa picha zake. I really admire you. Keep it up

Anonymous said...

haswa mama! umeongea POINT! wengi wetu we lack confidence kama wasemavyo wazungu . .. Mwanamke Hulka jamani; kama mmefika hapo ni jambo la kushukuru Mungu kwani dunia imechafuka mwenzangu .. .

Anonymous said...

sasa ukimtafuta matron mbaya si picha zitaharibika. mi nafikiri ni swala lakujiamini, bi harusi ni ba harusi habadiliki ilimradi apate wapambe wazuri wanaojua kupamba. Ukishtukia matron ni mzuri zaidi yako we omba kumeremeta zaidi itakuwa poa tu.

Anonymous said...

Kwanza Shamimu nakupongeeza ulipendeza!! Pili kuhusu matron "mbaya" kwanza ina maana gani? Mara nyini watu huchukua mtu ambaye kidogo wanalingana kiumbo, kimo na mvuto ili wote muwe na mvuto. Mie nadhani hao wanaosema wachague matroni mbaya hawajiamini kabisa. Na jingine wengine hupemda kuchukua matron ambao wapo ktk ndoa yaani mume na mke.........

Anonymous said...

tuwekee za send-off au kitchen party tugune. hapo umemzeesha au kajizeesha kwa mtandio?

Anonymous said...

Shamim naomba uniweke sana unaongelea uzuri wa matron au matron kupendeza zaidi ya bi harusi. Mimi naonelea hivi, hata matron awe mzuri akuzidi kiasi gani kama wewe umeji-DECORATE zaidi yake na nguo yako ni zuri zaidi yake lazima utakuwa bomba tuu haijalishi yeye mzuri. Pale watu hawaangalii uzuri wanaangalia mapambo...

laurel said...

hapo umetukata ulimi hata sie waosha midomo maana nilizania haujaolewa(joke)haya ndio mambo lazima uwaonyeshe mfano na wao wafuate poa sana more photo kama mdau hapo alivyosema ,ulipendeza sana na hata wasimamizi,take care

Anonymous said...

Shamim tatizo sio kwamba mtu hujiamini ni kwamba mwanadamu unataka upendeze kwenye big day yako kila mtu apige "wooow" atleast ndo navyotaka iwe kwangu hivyo, anyway kwa kumchagua metron mbaya sababu eti unaogopa kupitwa hiyo ni HELLLLLLLL NO. Chagua metron mzuri, yah atapambwa lkn hato pambwa akushinde wewe. Mimi dada zangu woote wameolewa na metron wao woote walikua wazuri na bado dada zangu ndo waliisifiwa sana sababu wana natural beauty na hata hao ma metron walikua wazuri lkn ni vile jinsi ma biharusi walivyo pambwa ilikua tafauti na metron. Hata wkenye mavazi sijui kp/send off hutakiwi kuvaa sawa na metron atleast kaa mbali kwa mshono kidogo, harusi nyingi za bongo ninazo ona kwako hapa kwamba metron anapendeza kwa gauni la KP au SO kuliko bi harusi. Lakini tuarudi tena pale pale huwezi kumlaumu metron. Halafu hii sio kwa wabongo hata huku pia watu hawapendi ma metron wao wawazidi kwa hiyo its all women, but i think if i get married i'd want all my girls to look beautiful because they present me on that day. HELLLLL YES I ll be more beautiful bt they gotta look right too.

Anonymous said...

Jamani tuwe wawazi na wakweli bibi harusi ni siku yake anatakiwa apendeze sana na zaidi kuliko matron wake hii habari wewe si mrembo saaana harafu unaenda kuweka matron mrembo wa haja hata akipambwa kidogo tu anakuzidi ndo nini hiki tena
for me sichague best mbaya lakini angalau tukiwa mie na yeye isiwepo tofauti sana

lol
ni mtazamo wangu huo
J

Anonymous said...

okay, so mtu akinifuata kusimamia arusi apo najua duuh kumbe mi si bomba kama yeye, apo natoka nduki

shamim a.k.a Zeze said...

HAHAHA SHUKRAN....HARUSI YANGU ILIKUWA JANUARY 7 2007 WATERFRONT ndo ...mie wasiku nyingi kiasi ...KUNA MDAU hapo alihoji matron wangu kuvaa mtandio ENZI HIZO NDO ILIKUWA JUU...

so hata album zimejaa vumbi kama zi kuzeeka kwa picha

NISHASHUHUDIA SIKU MOJA NIKO SALON BI HARUSI AKAKATAZA MATRON WAKE ASIREMBWE SAANA.... BUT MWISHO WA SIKU YULE AMBAYE HAKUREMBWA ALIONEKANA MREMBO ZAIDI...SO HATA UKIREMBWA SAANA KAMA SIO, SIO TU...NDO MAANA NASISITIZA KUJIAMINI KUWA WEWE NDO BI HARUSI

KAMA MJUAVYO UZURI WA MTU UPO KWENYE JICHO LA MHUSIKA...WE WAWEZA SEMA UKO BOMBA KUSHINDWA MWENZIO MWENGINE AKAONA TOFAUTI

MARA NGAPI NIMEWEKA PICHA HAPA MIE NAONA NITAWAFUNGA MIDOMO...BUT KUNA WATU WANAONA HOLLA.

SO HAUWEZI MBANIA MWENZIO ASIREMBWE ULI UPENDEZE WEWE KUMBUKA UZURI HAUAMI WALA HAUAMBUKIZWI...MJIAMINI TU WATARAJIWA

Anonymous said...

kwani lazima uwe na matron?
nadhani hiyo mila ya matron na maids tuiiga kwa westerners lakini tofauti yao ni kuwa wakishatoka kanisani .....maids na matron kazi yao huwa imekwisha...
hawakugandi saa zote kaa wanavyo ganda wa kwetu.
na matrons na maids hukaa kwenye meza tofauti na biahrusi wakati wa reception, na pia hawavai nguo ya rangi moja

laurel(sis) said...

hapo ndio napo kupendea sis waambia mambo kwa wakati hata hizi za siku hizi baada ya miaka kazaa wataonekane walichemsha,za mama zetu tunaziona bomu lakini enzi hizo inaweza kuwa tolk of the town,halafu kama ni waterfront enzi hizo mwali ulifanya mambo.poa sana aliyetaka picha za send off mpe ajionee na hata ya shemeji mpe (lakini asije mtafuta )usimpe mambo yako poa anataka kuguna nini ndoa inakata miaka,mbona ataguna sana

Anonymous said...

shamim poda ilizidi kisdogo on your wedding najua too late huwezi kuchange but its just fyi
nakupenda zeze usije ukanijibu maana siku hizi tukikuchokoza tu unatutolea uvivu lol

Anonymous said...

shamim umeolewa juzi juzi tu kumbe watu walikuwa wanachonga eti umeolewa since 2005 ..wakawa oh shamy hana mtoto etc kumbe ulijipa tu muda wa kuenjoy na mumeo..safi sana..haya tunataka sasa kumuona na mr umembania sana..

Anonymous said...

MATRON ANATAKIWA KUWA RAFIKI YAKO WA KARIBU SANA, AWE MZURI, AWE MBAYA, AWE MNENE, AWE MWEMBAMBA. MTU AMBAYE MMESHIBANA. MIE MATRON WANGU ALIKUWA MTU AMBAYE NIMESOMA NAYE TOKA PRIMARY. SIKU HIZI NAONA WATU WANAKOSISHA HADI MATRON NA WANAONDOA KABISA MAANA YA MATRON. YAANI SHAMIMU 2007 NDO UNAONA ZAMANI? NA SIE WA 2000 TUSEMEJE?

Anonymous said...

Shamim mie cjawah muona huyo shem wetu mbona we tu kla cku tletee pcha mkiwa wote jamen

Anonymous said...

japo nimechelewa saana kucomment lakini mi naona bi harusi ni bi harusi apendeze asipendeze matron atabaki kuwa matron tu hata kama kapendezakiasi gani, mi nawashauri ma bi harusi wachague matron ambae wanaelewana sio eti umchague sababu umemzidi uzuri/urembo. sababu wahudhuriaji wa shughuli hawaishi kusema wengi wetu huenda kwenye sherehe kutoa kasoro si kusherehekea jamani mnaionaje hii