Friday, January 15, 2010

KWA WATARAJIWA


Mamboo mashost nimepata maombi kadhaa yakiniomba niwasukumie mavazi ya harusi wedding dress...nimejaribu kusaka fashion za kisasa na nimejaribu kuonyesha old fashions
KUHUSU RANGI YA MWAKA ESPECIALLY KWENYE MAHARUSI.....KWA KWELI BADO SIJAPATE JIBU KAMILI LABDA MWENYE UJUZI NAZO ATUANDIKIE ila mie napenda apple Green, baby Blue, Hellow!! i love this style...huyu ni bi Harusi Lady Jay Dee aliamua kutoka na style ya pekee

Mh hii plz its too old fashion....Usiifikirie kabisa na hili joto letu la bongo ndo kabisa labda waulayaaa
Kama hii imetulia mshono wa juu lakini hiyo mshono wa chini..aka sijapenda
Hii nimependa kuanzia juu na ilivyobana...hata huku chini tausi style sio mbaya...BUT.....
Woa ningekuwa mie i'll go for this simpla and classic

Huyu nae mshono wachini ni wa bibi harusi wa ZAMANI .....Cinderela style...ila kapendeza
...LOL....no comment nasubiria kutoka kwenu.....
Hiii sio mbaya lakini ataevaa awe mreefu au avae viatu virefu ili hiyo style ya chini ionekane....mshono wa mikono hii wanashona kwa wale kanisani ambao hawa

16 comments:

Anonymous said...

sup shamim! aisee kumbe ulipendeza ivo sasa mbona umekandamiza sana ma misosi sa hizi sio model tena anyways u stil luk gud..bout magauni ya harusi cinderella is so much in fashion if u dint know na juu inakuwa tube lakini naomba ututaftie zaidi wedding gowns utuwekee mpenzi wengine tunaolewa ivi karibuni?je shamim maduka mazuri wapi ya vipodozi nataka kung`arisha uso kidogo sio kujichubua bt nakuwaga na pimples kidog so natumia dawa ya kuondoa...plz advise. alafu duka lako liko sehemu gani na price zinakwendaje

sophia said...

Shamim mbona hayo magauni ya Cinderella unasema ni ya kizamani basi huku Marekani hayo ndiyo yenyewe ya watu wenye pesa zao, sasa hayo ndio bei mbaya, hivyo vigauni tight bei ya kawaida tu. Mimi harusi yangu lazima nitoke na Cinderella I dont care huko bongo mkiliona la kizamani.

Anonymous said...

Cinderella style is the only one dat I liked...and ur dress too Shamim...I like it as well...Keep it up

Anonymous said...

Ni kweli kabiza cinderella fashion iko juu bado..
Shamim hata wewe pia ulipendeza kwenye harusi yako ....jamani kazana na diet ure- gain figure yako bwana

sophia said...

Shamim kwenye harusi yake alipendeza. Simple N hot. Hapo Shamim alikuwa mwembamba na alipendeza. Lakini jamani mimi mbona nimemuona last month ni kweli kaongezeka lakini sio kama vile watu wanavyosema kwenye hii blog. Sio mnene wa hivyo, yupo tu wa kawaida wala hachushi, akivaa anapendeza.

sophia said...

Mimi mwenzenu JD nampenda sana tabia yake, nyimbo zake napenda, na ana sauti nzuri sana tena ya natural sio wengine wakiimba mpaka wajikakamue au wabadilishe sauti mara wabane pua. Lakini mimi mwenzenu style zake za mavazi MMMH! Harusi ni tukio kubwa sana katika maisha ya mtu, kivazi alichovalia katika harusi yake mimi siamini. Lakini bwana kila mtu na taste yake.

Anonymous said...

LOl najua hayanihusu,lakini vivazi vyooote hivi shamim lakin hiki cha Jide ,akha mwenzangu akijanikolea machoni mwangu .Lol wala siamini kama alivaa hivyo kwa wedding yake am sorry lakini hakupendeza,ahh watu wanapenda kuwa different but this was too much,nope not for me.Babes ulipendeza.

Anonymous said...

kweli dada sophia umejaliwa na mawazo, hongera kwa hilo. .. ni kweli dada jd vazi alilovaa harusini sio mwake kabisa. sasa sijui kaingia kanisa gani yailah toba wanaloruhusu mambo hayo.!!! ila ni choice yake mwenyewe.cinderela ipo kwenye chat kabisa dada shamim. ila umependeza sana kwenye harusi yako.

Anonymous said...

JD hakupendeza jamani...

julie said...

Kweli hata mimi JD kanishangaza sana. Picha yake ya harusi mimi niliiona mara ya kwanza kwenye blog ya michuzi. Alikuwa ametoa hicho kikoti cha juu akawa amebaki na hicho ki-top kimekaa kama sidiria. Nilishangaa sana. Lakini mimi huwa nasikia JD ni mmoja kati ya wanamuziki wanaojiheshimu sana. Sasa nashindwa kuelewa. Kama alivyosema Sophia hapo juu, "Harusi ni tukio kubwa sana katika maisha ya binadamu". That is very true nakubaliana naye kabisa. Hivi kweli wazazi wake, wakwe, ndugu, jamaa na marafiki wanakuja kwenye harusi yake wanamkuta yuko hivyo?! Kwa kweli hapana that is more than too much!

tabu said...

Shamim ulipendeza,
Nimeipenda yako,simple bila vikolombwezo vingi.
Hiyo ya mwisho kwa mtu mrefu aliyenyooka inapendezea,

Anonymous said...

Unajua hapa bongo tunakatabia cha kutaka tuwe au tuonekane exceptional especially kwenye weddings and the like.Sasa sishangai sana Kivazi cha Jide,alidhamiria in my understanding afanye kitu exceptional labda hata hamna aliyewahi kufanya Bongo.All in all hajapendeza hata kidogo katia aibu tu,lakini kwa status yake nadhani family yake ilishindwa kumshauri.Bongo kuna mambo.

Mija Shija Sayi said...

Shamim mbona hujachukua fomu?

Fanya haraka karibu zinaisha, pitia hapo chini.

http://www.blogutanzania.blogspot.com/

shamim 'Zeze' said...

Ahsanteni wapendwa kwa maoni yenu ndo yanihamasishayo,,nikaze buti

Kuna mrembo ambaye ni mtarajiwa alitaka kujua duka langu lilipo lipo sinza Mori kwamaelezo zaidi tuwasiliane ...ndo tutashauriana kuhusu mambo ya kung'aa uso nk USIGUSE MKOROGO PLZ shamyomy@yahoo.com..

Da Sophy plzzz mimi sintokushauri uvae cinderela style na hiyo shape kwanini uifiche...show what ur mama gave ya!!...hiyo style is done plz ladies u have to understand japo ni nzuri lakini sio kwa sasa

But what can i say as long as kila mtu she has her test ndo maana JIDE aliamua kuvaa hivyo na wengi mko agaist...ITS HER CHOICE!!

No comments:

Post a Comment