Saturday, March 20, 2010

JAMILA’S KITCHEN PARTY


BRIDE::JAMILA
VENUE::DIAMOND JUBILEE VIP HALL
COLOR::RED & GOLD
MC::DELILA
DECOR::GLORIA DECORATION



Hii alovishwa bi harusi jina nimesahau ajuae atatuambiwa...nilidhani mwanzo mbwembwe itafika kipindi bi harusi atafunuliwa....weee nikaambiwa sioni sura Ngooo hadi siku ya kuolewa huyo mchumba wa mtu bibi kuonesha onesha sura inahusu??!!

Ukumbi ulikuwa umenooga kwa style hiii

Somo akiwa kazini na mwali wakee
Mama wa Bi harusi Saida China.....akimuongoza mwanae...Rahaaa
Somo akimuandaa mwali wake babla ya kuingia ukumbini

Bi Harusi na Dadake......Kulikuwa na suprise....Kideoni kaka mtu akiwa sambamba na dada wake wakampa tip Bi Harusi...zote mbwembwe tu!!

Kuingia tu mama akaanza kumuosha mwanae na mijihelaa...
Huyu ndo Mwenyekiti wa kamati upo hapoooo..

UKAFIKA MUDA WAKUTUNZANA
Somo nae alitunzwa na Mamaa Saida China
Wado zake Saida wao walitunza madafu na dolariiii....shurti wamezifunga taji
hahahah huyu Saida China bwana.....Mabizness Women wenzie wakamtunza pesa ya China...CHEZE





Somo ndo aliyelianzishaaa....hakuna kutunzana jasho kwa Kanga na vitenge hapa ni mijihela tu mwanzo mwishooo....wink
MC...alikuwa Delila
Hii ndo ilikuwa kadi ya mwaliko sambamba na Menu!!


hii chai na cake (ina zabibu na nuts ndani yake )tulipewa saa kumi kabla ya kula...Sekela , Mbuzi choma na ndizi.....Maana hii Party ilianza mchana ambako watu walianza kula Lunch..upo hapo mie sikuwepo nililetwa usswahili wangu wakudhan ukiambiwa saa 6 uende saa kumi....
UBUNIFU NDO HUU
SOMO Bi Zulekha wa Sum Super Stoo...nae alikua na zawadi za kumtunza Bi harusi wakee..upo hapo

Somo huyoo Quran muhimu kujisomee...Somo alimtunza hiki mahsusii

Lol ...hadi napost picha sijajua hiki ni kitu gani...mambo ya Somo hayooo
Mzigo huu ulikuwa kutoka kwa mama...yaani ile stage ya juu ilikuwa imefunikwa...'Mama akatoe zawadi kwa mwanae...nashangaa camera man wanakimbilia kule .mara ohoooooo utasema duka la fenicha.....lakini zilikuwa zawadi za Bi jamila toka kwa mamaake...rahaaaa




KULIKUWA NA SASAMBU SASAMBU YA KABATI NA SI SANDUKU...DADA MTU NDO ALISIMAMIA ZOEZI
mambo ya kisauz nayo yalikuwepoo...siwajua mambo ya Zuma zuma....
Melody ndo walikuwa wanarindima siku hiyo balaaaaa




RED CARPET

































No comments:

Post a Comment