Thursday, March 25, 2010

OSSY BAG PARTY

EVENT::BAG PARTY
GROOM::OTHUMAN 'OSSY'
VENUE::VIJANA HALL
COLOR::BLACK & WHITENITOE SHUKRAN KWA KUALIKWA JAMANI...SIKUWAHI KWENDA KWENYE BAG PARTY HII NDO YAKWANZA KWENDA...ILIPENDEZA...NIKAGUNDUA KUMBE BAG PARTY NI WANAWAKE WANAMTUNZA KIJANA WAO ZAWADI...KAMA ILIVYO KITCHEN PARTY WANAUME SI WEENGI ...UNLESS KAMA NI HII TU ZINGINE NA WANAUME HUALIKWA...mtanijuza zaidi......KWA KIFUPI ILINOGA too sad hakukua na JIUGONJWA...nilikuwa na hamu nione inafananaje......i think ingeweza kuwa ya SANDUKU/BEGI HIVI....lol

OSSY ALIKAA PAMOJA NA NDUGUZAKE NILIPENDA HII IDEA NINAVYOJUA WANAUME WENGI WANAKUWA NA NOMA KUKAA KWENYE KUNDI LA WANAWAKE...LAKINI HAWA WALIKUWA 6 HIVYO WALIKUWA WANAPIGA ZAO STORY....na wengine wakiwa wanachat na simu zao....wink very interesting!!

MAPAMBO
zawadi alizokabidhiwa Ossy.
Mama Ossy Anafanya kazi Tanesco wafanyakazi wenzie ndo walikuja shereheka nae
Nilifurahi kukutana na MC wa kitchen party yangu Mc Maselina nae alikuwa MC mwalikwa
Kuna hii style ya kutunzana.....especially ikiwa mtu anatuzwa kanga anazungushiwaaa kama pea kumi, na hili joto la dar ukumbuke mtu yukoe kwenye tension, kuna siku mtu anakuta zimia.....si mumpe mkononi au aweke kando.....napenda Style ya Somo Zulekha ya kutunza anazipanga kwenye kitenga na kuzifunga kama gift......ni UBUNIFU TU

HUYU MAMA ALIKUWA KACHANGAMKA SAANA...NAPENDA WATU KAMA HAWA KWENYE SHUGHULI......UNAJIACHIA KWA RAHA ZAKO SIO MTU ANAKUJA KWENYE SHUGHULI KANG'ANG'ANIA KWENYE SITI KAMA KATIWA GUNDI....HANYANYUKI KWENYE TAARAB WALA MAPAMBIO...si ungelala Nyumbani?!!
MAMA OSSY!!

raha ya shughuli kucheza na kucheza kwetu muhimu kuduwarishaaaaa...
mduara na ndo huooo

na Huyo ndo alikuwa MC alikuwa anajipa raha mwenyeweee...kwa raha zakee
tulichezewa na kiduku siku hiyooooo

Mama Kova nae alikuwepoooo!!
Tamalaa UK upo?!! salamu zakooo...toka kwa Aunt Zulfa
Kama kawaida Mtoto wa Somo akanisuprize...nikauliza hili nini tenaa..."nikaambiwa Kasha bibi ya kuhifadhia nguo...hatutaki beba fungo la Rambo sie"...wink
MI NILIVYOONA HILI NILIJUA NDO MABEGI YENYEWE...lol
Mbwebwe za msisitizo wa Rangi...chezeyaa

mashost nao walimuosha shoga yao Zulfaaa.....!!
Lisa na kati ya Nyumbani ni Nyumbani tbc1....NILITAMBUA UWEPO WAKOOO...salamu ziwafikie HUKO SWEDEN!!
Shost alikuja toa zawadi kwa niaba ya Lissa....

Salma Mtoto wa Somo nae akambeep mama ake...kwa kile kidude cha kufukizia nguo.....picha zake zaja za harusiiiiii...endelea kuperuzi 8020 FASHIONS
bila shaka tushajua matumizi yake...unakitaka kidude tuwasiliane nikupe Mchongo!!


SAMAHANINI WADAU SIKUWEZA NASA RED CARPET VYEMA NILIFIKA LATE...si mwajua tena majukumu?!!






haya mabazee ndo yalikuwa sare.........yanapendeza!!

No comments:

Post a Comment