Saturday, March 20, 2010

MJADALA:: BI HARUSI KUVAA SARE NA MATRON

MJADALA:: BI HARUSI KUVAA SARE NA MATRON

Tumekuwa mashuhuda wa nyingi za Kitchen party kuona mavazi ya bi harusi mtarajiwa akiwa yamerandana na Matron wake kuanzia kitambaa, rangi ...ikitofautishwa kidooooooogo na mishono wanayoishona...

huku Matron akiwa kashonewa Simple na nguo ya Bi harusi ikiwa imetiwa masham sham na nakshi nakshi zaidi katika kuwatofautisha.Kitu kinachopelekea Matron aonekane mtanashati kushinda Bi harusi.

Je wewe kama mdau unaonaje hili..ni bora wavae rangi tofauti na mishono pia tofauti au sababu Mishono mara nyingi huwa tofauti lakini mwisho wa siku hatuoni tofauti au kipi kifanyike Ili Bi harusi aonekane tofauti na Matron??!!

hapa waliamua kuvaa wote sari ila rangi tofauti ...je imetulia au la?!!
Hawa walivaa kitambaa kimoja ila mishono na nakshi nakshi tofauti ...je umemsahau bi harusi?

Hawa nao kitambaa kile kile ila mishono tofauti..je we haijakupendezaaaa?!!

Hii ndo ilikuwa kali kabisa ni bi harusi na matron ...lakini rangi na hata mishono ni tofauti kabissaaa....hivi ndo nyie mnavyotaka?????!!!

23 comments:

shamim a.k.a Zeze said...

KAMA KAWA NAOMBA NIFUNGUE MJADALA

MIE NIMEKUWA SHUKUDA WACOMMENT NYINGI WATU WAKISEMA MATRON KAMFUUNIKA BIHARUSI....NA WATU WAKILALAMA KWANINI WANAVAA SARE



MFANO HIYO PICHA YA CHINI UNAWEZA KUSEMA HUYO NI MWALIKWA ALIENDA PIGA PICHA NA BIHARUSI ...LAKINI NI MATRON HUYO...HEBU ONA INAVYOKUWA HAIJATULIA...HAPO RANGI YA SHUGHULI ILIKUWA NI NYEKUNDU...LAKINI HAPO MATRON KAVAA BLUU....HATA PALE MBELE INAKUWA HAIPENDEZI KIMAPAMBO

SO MIE NAONA MATRON NA BI HARUSI WAVAE TU SARE ILA BI HARUSI ATILIWE NAKSHI NA AREMBWE VYEMA

MIE BADO NAAMINI BI HARUSI NI BI HARUSI TU UKIONDOA HAYA MAVAZI WANAYOYAVAA...KATU KUFANANA KWA MAVAZI HAKUTOBADILI MATRON AWE BIHARUSI.

Anonymous said...

mie napinga sanan mambo ya kuvaa karibu na sare. ebu angalia picha ya pili jinsi ambavyo huyo wa kushoto alivyopendeza. yaani msimamizi (matron) ametulia kimavazi kuliko minakshi-nakshi ya bi harusi watarajiwa.
mie nimemfurahia huyo aliyevaa rangi tofauti na bi harusi mtarajiwa. angalia picha ya nne.

Anonymous said...

hapana kwa kweli hiyo blue and red, hiyo ni kachumbari ya kutosha. pich ya kwanza ni nzuri na iendelee kuwa hivyo. nakubaliana na mchangiaji aliyepita.

Anonymous said...

kama utakumbuka wiki km 3 zilzopita uliweka bi arusi na matron wake mimi nikawa wa kwanza kutoa maoni kuwa mbona inanonekana matron kamfunika bi arusi,anyway mimi naona saa zingine inategemea na mshono,wakati mwingine madesigner wanakosea jinsi ya kuweka nakshi nakshi mpaka nguo ya bi arusi inaonekana mbaya,mfano picha ulizotoa hapo leo kuna ma bi harusi wamependeza kuliko matron halafu kuna bi arusi wamefunikwa,nina mengi ya kutolea maoni c u later for more

Anonymous said...

Haya asante kwa mjadala mzurui

mie nasema hivi issue inakuja kuwa matron anatoa hela yake mwenyewe kwa ajili ya shughuli ya mwenzie ni wachache sana ambao wanawagharimia matron zao sasa hivi so mtu anaona hela yake kwani nini ashone midebwedo anataka na yeye apendeze!!

hapo ni mtihani jamani!! na pia watu wawe makini ktk kutafuta matron wao wawe washauri wazuri sio wale wenye maamuzi yao ktk kila kitu

Anonymous said...

MIMI BINAFSI NIONAVYO NI KWAMBA WAVAE RANGI SAWA LAKINI MATRON MAPAMBO KWENYE NGUO YAPUNGUE NA HATA HUKO SALOON MAREMBO YA MATRON YAPUNGUE

hafsah said...

mi naona wote yani bibi harusi na matroni washone sare kila kitu labda ktk kurembwa nywele na uso.apo bi harusi ndio azidishwe makeke.
hafsah aka Mrs.Hassan Kipende

Anonymous said...

Accoarding to my view, naonelea tena inapendeza kama bi harusi na matron wavae sana ila ya bi harusi iwe na NAKSI nyingi na mishono iwe tofauti pia. Ukisema wavae rangi tofauti haipendezi wala haileti maana cha msingi DESGNER awe makini kwenye ku-DECORATE hizo nguo. WATARAJIWA MPOOOOOOOOO.!!!!!!!!!!!!! IT YOUR TIME BABIES...!!

Anonymous said...

Kuvaa sare inapendeza mi niliwahi kuwa matron ila nilipata shida sana maana sikutakiwa hata kupaka wanja kisa nitamfunika bibi harusi, nashauri bi harusi wajiamini siku ya haruis ni yako utapendeza tu hata iweje pia mnaopata bahati ya kuwa matron tafadhali nawaomba mzingatie kilichokupeleka pale sio kuwa na intension ya kumfunika mtoto wa watu siku ya harusi yake au sendoff hata K/p na kama simple ndo inapendeza basi ma Bi harusi wapende kuwa simple si kuweka makorokoro mengi mwisho wa siku inakuwa mbaya

Anonymous said...

Shamim hata mi nakuunga mkono - sare inatulia na ina raha yake haswa katika kupendezesha mapambo kwa ujumla. Ama la kama watavaa tofauti basi rangi ziwe contrasting ila zinazoendana/ shabihiana kama wale waliovaa sari ile picha ya juu. Matron anatakiwa afifie kidogo amuachie bi harusi ang'are!

Anonymous said...

Nakubaliana na wewe mama Iqra. Mimi naona wavae kitambaa sawa na bi harusi aongezewe nakshi nakshi zaidi na atapendeza tu.

Anonymous said...

nakubaliana nawe da shamim. Ila, hii imekaaje? bi harusi akiwa peke yake kwenye high table? Mi nimepanga yangu iwe hivo....hebu nipeni ushauri dada zangu. Wapambe wangu watavaa sare, ila matron hatokuwepo.

Anonymous said...

Miminadhani swala la nakshi na masham sham ni matakwa ya mtarajiwa mwenyewe. Kwani huwezi kumridhisha kila mmoja. Ni bora mtarajiwa mwenyewe uridhike na kufurahia siku yako.
Swala la kufunikwa sometimes lipo kama ukimchagua/chaguliwa matroni mzuri kushinda mtarajiwa au matroni akiwa mng'avu kushinda mtarajiwa.

Anonymous said...

mi naona hapa swala ni kwamba watu hawajiamini ndo mana wanahofu kuwa matron atamfunika bi arusi.

mi naona wote wanahitaji kupendeza halafu kama ukichunguza kupambwa simple ndo inapendeza kuliko makorombwezo yakizidi na nguo iwe simple tu sio mapambo yanazidi mpaka inaharibika.

marton wengi wanapendeza kwasababu wanakuwa wamepambwa simple kiasi kwamba uzuri wao wa asili unaonekana zaidi ila bibi mtarajiwa anapambwa sana uzuri wote unafichwa behind make-up.

nilishawahi kusimamia send off ya shosti wangu na rangi ilikuwa maroon na white,shosti akasema yeye atavaa maroon mie nivae white mwisho wa siku mie ndo nilipendeza japo nilipambwa simple sana ila yeye alijaziwa mapambo mpaka ikachukiza wakati she is so cute without make-up

Anonymous said...

Anon hapo juu unayesema hutakuwa na matron hayo ni maamuzi yako as long unajiona utakuwa comfotable au may be unaogopa kufunikwa? Joke...!! me naona ni maamuzi ya bi harusi, unajua siku ya harusi uko huru kufanya chochote, ni siku yako na hairudiwi jamani, kwa hiyo jiskie huru kufanya vyovyote!!! kwa hiyo hao wapambe wako watakaa pembeni wapi? yani hawatatakiwa kukusogelea? mana wakishakusogelea ni yaleyale kwamba kama wapambe watakuwa wamependeza wanaweza kukufunika tu vilevile...

Esanja said...

Asaalam aleykum!mdau hapo juu uliyesema kuwa hutaki matron ila utakuwa peke yako hightable ila wapambe watavaa sare.Hiyo ni nzuri mi nishasimamia sendoff ikawa hakuwa matron na tukawa wapambe wanne na meza ilikuwa imerembwa kama round ila mbele maua yakazidi na ikabaki space ya mbele tu na ilipendeza saaana.Na kuhusu mjadala mi naamini bi harusi ni bi harusi tuu hawezi kwa matron.kitambaa kikiwa kimoja na mishono tofauti na bi harusi ikazidi nakshi ni sawa au mshono mmoja bi harusi akarembwa zaidi nywele na uso pia ni sawa.bi harusi hatakiwa kuwa simple saaana cz ni special day jamani hairudii tena.Na pia kwenye mkusanyiko wa watu wengi lazima dosari ziwepo as long as si ni wanadamu si malaika.hayo ndio maoni yangu wapendwa

Kyekuu said...

Mada ni nzuri, mi naona wavae sare na tofauti pia iwepo km walivyotangulia wenzangu kusema, la muhimu zaidi ni kuwa naomba watarajiwa wawe makini sn katika kuchagua mtu wa kumsimamia usichukue mtu aliyekuzidi uzuri, ss mtu unanyimwa hata kupaka wanja jamani, aka mimi matron wangu namchagua mwenyewe hata akipaka nn hawezi nizidi alaa.... kila mtu ni mzuri ila tunazidiana eti jamani ee?? ushauri wa bure!!!!!

Anonymous said...

Jamani tatizo la matron kumfunika bibi harusi linatokea pale ambapo bibi harusi na matron wanashona nguo kwa mafundi tofauti na wanaenda kurembwa saloon tofati kwa hiyo fundi na saloon anayoenda kurembwa matron wanaweza kuwa wataalamu zaidi ya fundi na saloon anayorembwa bibi harusi.

Anonymous said...

Zeze tatizo sio kuvaa tu sale naipitisha wavae ubaya inakuja ma biharusi wanapanikishwa na hao mafundi wanawkewwa nakshi ndio wanavuruga matroni ameshona simple anapendeza. na kingine cha muhimu nyie watarajiwa angalia msimamizi wako we unamchagua mtu kama nacy sumari au kina odemba unategemea watachukiza hao kirahisi aah angalieni bana kuna watu wengine wameumbwa na sura nzuri kama bi harusi umejicream ung'are au umekandikwa mapoda kukurembusha miwshowe unaonekana kinyago. Mjiamini na mmake goo choise za mavazi na wasimazivi sare ivaliwe ila isiwe common in each and everything. matroni zingine wanaushepu haswa then mnachagua mtindo wa marmaide sijui niseme nguva hapo bi harusi huna ziwa wala wowowo trust me utachekesha.Mnamkumbuka Chabba? mzimamizi wake na yeye walijulikana vika nani mwali nani anasindikiza lol.
Kingine mabiharusi watarajiwa msikuli kufunga ndoa mnamimba kubwaaa jamani ndio chanzo cha kutopendeza usoni na mavazi, hapo usimlaumu matroni akitoka bomba,

Anonymous said...

da shamy kwanza naomba nimsuport yule anaesema hataki kuwa na matron kwenye high table mimi nilifanya hivo kwenye harusi yangu nilikuwa mie na mume wangu tu matron bestman walikaa kwingine kabisa,,ilipendeza sana.
kuhusu matron na bi harusi kuvaa sare mie nakubali kitambaa au theme iwe inafanana except mishono. bibi harusi wengi huwa wana complicatiwa nguo na ku-over do make up ndo mana hawapendezi na wengi kama bibi harusi mweusi anachukua matron mweupe au vice versa hii pia huchangia labda bi harusi kufunikwa. ushauri kitambaa kiwe sare, mshono wa biharusi uzidi wa matron na bi harusi always kumbukeni msichukue ma matron wazuri zaidi yenu ..
PS:zeze wewe siwezi kukuweka matron hata siku moja binti wa kimachame ahahaha(joking)

Anonymous said...

Mi naona wavae rangi sawa watofautishe kidogo,unajua si wanawake tunajua ukiwa bibi arusi tafuta matron ambaye hatakufunika yaani kwake uonekane better off.ila wenye blue na nyekundu wamechemka haijapendeza.

Anonymous said...

Jamani.Ukitaka kuolewa matron sio necessarly awe rafiki yako.Ni mshauri wako.Sasamshauri huyu mchukue ambae si mzuri kupita wewe mzizi wa fitna utakatika ila sare wavae maana uzuri wako bi harusi utashine up

Anonymous said...

Sawaa wa hapo juu,mimi kwenye harusi yangu nilimuweka matron mtu mzima about 50 na mimi nai 30's tena yeye ni mzungu,na kama unavyojua wazungu hawajirembi hiivyo at least akiwa 50's aah kwa raha zetu nguo sare sare kila kitu

No comments:

Post a Comment